content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
SERIKALI ilitenga Sh bilioni 54.5 kugharamia mafunzo ya ndani na nje kwa watumishi wa umma nchini katika mwaka 2017/18 pia imetenga Sh bilioni 39.8 katika kipindi cha mwaka 2018/19.Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Dk Mery Mwanjelwa ametoa takwimu hizo wakati kijibu swali la Mbunge wa Kuteu...
kitaifa
RAIS John Magufuli amewaweka kikaangoni wakuu wa mikoa ambayo haijaanzisha masoko ya madini na kuwapa siku saba wawe wametimiza agizo hilo, huku akiwaonya pia viongozi wote wasiotekeleza maagizo yake.Kauli hiyo aliitoa jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wilayani Chunya baada ya kuzindua barabara ya Mbey...
kitaifa
WAWAKILISHI pekee nchini kwenye michuano ya kimataifa, Yanga, wanatarajiwa kutoana jasho dhidi ya Pyramids ya Misri katika mchezo wa ply-off kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Kombe la Shirikisho Afrika katika mchezo utakaopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.Yanga awali ilishiri...
michezo
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani (UDSM) kinatumia maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) kueleza namna ya kutumia majani ya miwa katika kutengeneza karatasi.Mtafiti kutoka UDSM, Said Issa alisema hayo Dar es Salaamjana katika banda la UDSM lililoko katika maonesho hayo maarufu kama sab...
kitaifa
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustin Mahiga amekitaka Chuo cha Diplomasia nchini kutoa mafunzo mtambuka ili kukiwezesha chuo hicho kuzalisha wahitimu wanaoendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.Mahiga aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa mahafali ya 28 ya chuo hicho na...
kitaifa
['Tottenham wanasuka mipango ya kumrejesha mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 30, kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwishoni mwa mwezi. (Express)', 'Manchester United wanaweza kumtimua kocha Ole Gunnar Solskjaer iwapo matokeo yao hayataboreka msimu huu, huku kocha timu ya taifa ya England Gareth Southgate akip...
michezo
MAENEO takribani 9 katika hotuba ya Msemaji Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jana, yalikataliwa kusomwa na Kiti cha Spika kutokana na kukiuka taratibu za Bunge.Kabla hajaanza kusoma hotuba yake, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu alimtaarifu Msemaji wa ka...
kitaifa
KAMATI ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe imesema itamkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani orodha ya majina ya vigogo wanaoendekeza tabia za kula rushwa kutoka katika taasisi zote za serikali ikiwamo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).Mweny...
kitaifa
MKUTANO wa Rais John Magufuli na wafanyabiashara umeibua mambo mazito ikiwamo udanganyifu na ukwepaji kodi unaofanywa na wafanyabiashara huku baadhi ya taasisi na watendaji serikalini wakinyooshewa vidole kuchangia hali hiyo.Kwenye mkutano huo uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana ambao Rais Magufuli alisema ana...
kitaifa
TIMU ya Taifa ya soka ya wanawake chini ya umri wa miaka 17, leo inatarajia kushuka kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza na timu ya Burundi katika mashindano ya kufuzu Kombe la Dunia 2020 nchini India.Mchezo huo ambao ni wa hatua ya awali unatarajiwa kuwa na ushindani kwa sababu timu hizi zinafahamiana na mara...
michezo
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa kongamano la pili la biashara kati ya Tanzania na China juzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye alisema taasisi hiyo inakaribisha wawekezaji kutoka nchi hiyo katika juhudi za kufikia maendeleo endelevu hap...
uchumi
Katika hafla hiyo ya chakula cha usiku iliyofanyika hoteli ya Serena, wafanyabiashara hao wa makampuni makubwa hamsini ya Ufaransa wakiongozwa Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak walikula huku wakitumbuizwa na mwanamuziki gwiji nchini Zahiri Ally Zoro.Akizungumza kabla ya kukaribisha wageni wake katika chakula hic...
uchumi
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa mfumo huo unaotarajiwa kuanza mwaka huu utasaidia wakulima kuwa na soko la uhakika, bei nzuri na inayostahili. Alisema hayo baada ya kufungua warsha iliyolenga kuzungumzia mfumo wa soko la bidhaa, faida na changamoto zake.“Ni kwa kufanya hivi nd...
uchumi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Dk. John Pima amesema eneo hilo ni la kimkakati kibiashara na kiuchumi.Amesema, Kaliua ni 18.8% ya eneo la mkoa wa Tabora, linafaa kwa uwekezaji kwenye sekta mbalimbali, kuna malighafi za kutosha na miundombinu rafiki.“Tunazo fursa nyingi kwa Kaliua , nyingi sana...
uchumi
KIFO cha bilionea maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki na mmiliki wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi, kimewashtua wengi, huku akiwa ameacha pengo kubwa katika maeneo ya biashara na vyombo vya habari.Dk Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni hayo ya IPP, alifariki dunia usiku wa kuamkia jana Du...
kitaifa
TANGU Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani ikiongozwa na Rais John Magufuli, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeonesha ari na kasi kubwa zaidi katika kurasimisha makazi mijini.Hali hiyo imeiwezesha serikali kuongeza mapato yake kupitia ukusanyaji wa pango la ardhi, ada na tozo mbalimbali zitokana...
kitaifa
KUNA uwezekano mkubwa kwamba miongoni mwa watu wazima wanaopata maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya homa ya ini B, hupona kutokana na afya ya miili yao, Imeelezwa. Aidha, imeelezwa pia kuwa watu hao baada ya kupona kupitia kinga yao ya asili kupambana na kuviua virusi hivyo, hatimaye miili yao hujitengenezea kinga ya ...
kitaifa
NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (pichani) amesema ifi kapo Julai mwaka huu, jiwe la msingi litawekwa kuashiria kuanza kwa utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa ufuaji umeme wa Mto Rufi ji maarufu kama ‘Stiegler’s Gorge’.Hayo aliyabainisha bungeni jana wakati akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge kwenye baj...
kitaifa
MABINGWA wa soka Bara, Simba wanatarajiwa kuweka kambi Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.Simba inayotarajiwa kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, juzi ilitangaza orodha ya wachezaji 27 iliyowasajili kwa ajili ya michuano mbalimbali. Kwa mujibu wa ofisa habari wa Simba...
michezo
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amesema hatowavumilia watumishi wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo watakaokwamisha wafanyabiashara na wawekezaji wenye viwanda na kuwahimiza watumishi hao kuwa wawezeshaji.Aidha, amesisitiza haja ya kuja na sera maalumu itakayounganisha sekta za kilimo, biashara na...
kitaifa
SERIKALI ya China kupitia Jeshi la Ukombozi la China, kikosi cha Anga limetoa msaada wa ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Taifa kilichopo Kunduchi, Dar es Salaam unaogharimu Shilingi Bilioni 56.Ujenzi huo wa awamu ya pili ya chuo hicho utakifanya kuwa cha kisasa na miundombinu rafiki na kukiwezsha chuo hicho kud...
kitaifa
Utekelezaji wa mfumo huu unafanyika kutokana na kubainika kuwa na mafanikio makubwa baada ya majaribio yake kufanyika tangu Julai mwaka jana.Unalenga kupunguza gharama na kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki, hali ambayo itavutia uwekezaji katika nyanja mbalimbali za uchumi.Ina...
uchumi
Huduma zinazotolewa na duka hilo ni pamoja na kukusanya ankara, kurudisha namba zilizopotea, mauzo ya simu, kutuma fedha, kusajili namba na huduma za kimitandao. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jana, Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja wa Airtel, Adriana Lyamba alisema ”uzinduzi wa duka hili ni uthibitisho ...
uchumi
WALIONYANG’ANYWA taa za sola na jenereta wakati wa oporesheni ya kutokomeza uvuvi haramu nchini watarudishiwa zana zao bila masharti yoyote.Kauli hiyo aliitoa bungeni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wakati akitoa maelezo ya nyongeza kwenye jibu la Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Abdallah Ulega aliyekuwa akijibu s...
kitaifa
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora ipo kwenye mchakato wa kujenga kiwanda cha asali na inakaribisha wawekezaji wa viwanda vya bidhaa zinazotokana na zao hilo la nyuki.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Martha Luleka amesema, kiwanda hicho kitaongeza thamani na matumizi ya asali inayozalishwa kwa wing...
uchumi
TANZANIA imepaa kwa nafasi mbili kwenye ubora wa viwango vya Fifa vilivyotolewa jana na sasa inashika nafasi ya 135. Kwa mujibu wa viwango hivyo, Ubelgiji bado inashika namba moja ikifuatiwa na mabingwa wa dunia Ufaransa, Brazil ikishika nafasi ya tatu, England ya nne na Ureno ni nia tano. Kupanda kwa nafasi mbili za ...
michezo
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba leo wanashuka dimbani kuwakabili Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa ligi hiyo utakaochezwa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Mchezo huo ni muhimu kwa Simba kama itashinda itafikisha pointi 81 katika michezo 31 na kuishusha Yanga iliyokaa kwa muda mrefu k...
michezo
VINARA wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Yanga wamesema mchezo wa leo dhidi ya Alliance hawana budi kuja na mbinu tofauti na ile waliyotumia katika mchezo uliopita wa Kombe la FA dhidi ya Namungo kutokana na aina ya timu wanayocheza nayo.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 10.00 jioni kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza....
michezo
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amewasha umeme kwa ‘Babu wa Kikombe’ Mzee Ambilikile Mwasapila eneo la Samunge wilayani Ngorongoro Mkoa wa Arusha.Dk Kalemani amewasha umeme huo jana nyumbani kwa Mzee Ambilikile katika Kata ya Samunge, na kueleza kuwa serikali imetoa Sh bilioni 28 kwa Mkoa wa Arusha kwa ajili ya ...
kitaifa
TIMU ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano ya 17 ya dunia inatarajia kuagwa jijini Arusha Septemba 23, imeelezwa. Tanzania katika mashindano hayo ya Dunia yatakayofanyika Qatar mwaka huu kuanzia Septemba 27 hadi Oktoba 6, itapeleka wanariadha wanne tu, watatu wakiume na mmoja wakike, wote wakishiriki mbio za ma...
michezo
Aidha, mkutano huo ambao kwa mara ya kwanza utafanyika jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine utapambwa na maonesho mbalimbali ya bidhaa zitokanazo na zao hilo.Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo, Dk Herman Moshi, alisema tafiti zinaonesha kaya nyingi za Wata...
uchumi
Wamesema hatua hiyo itaongeza mitaji, pia kutoa hamasa kwa wanachama kupata mikopo mingi zaidi itakayowasaidia katika shughuli za kiuchumi.Meneja wa Saccos hiyo, Abbas Rajab akisoma taarifa ya Saccos kwa Rais Jakaya Kikwete, jana kabla ya kuizindua, alisema Saccos hiyo yenye wanachama 1,779 kati ya hao wanawake wakiwa...
uchumi
UJENZI wa gati namba moja katika Bandari ya Dar es Salaam uliokuwa ukamilike Desemba mwaka huu, umekamilika mwezi mmoja kabla hivyo kufungua milango kuanza kuhudumia meli kubwa nyingi zaidi.Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana ilisema gati hiyo imejengwa kisasa zaidi na kuvutwa ndani ya maji kwa ukubwa wa mita 200, ...
kitaifa
MFANYABIASHARA Rostam Aziz, Kampuni ya GSM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete wameichangia Yanga zaidi ya Sh milioni 500 katika hafl a iliyofanyika Dar es Salaam jana.Katika hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam na Waziri Mkuu Majaliwa akiwa mgeni rasmi, GSM...
michezo
VANILA ni zao linalojulikana zaidi mkoani Kagera kama ‘dhahabu ya kijani’ kutokana na kuwa mkombozi wa wakulima wengi. Hii ni kwa kuwa, ukiwa na miche japo mitano, ni kama vile tayari una dhahabu shambani kwako.Tangu mwaka 2015 dhahabu ya kijani (vanilla) imekuwa mkombozi hali iliyochochea kasi ya kilimo cha zao hili ...
kitaifa
OFISA Maendeleo ya Jamii katika Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Sophia Swai amesema wamebaini mbinu mpya ya wazazi kuwakatisha watoto wao wa kike masomo. Watoto hao wanakatishwa masomo ili wakafanye kazi za ndani kwa kuwazuia wasiende shule kwa makusudi kwa siku 90 ili waandikwe mtoro wa kudumu na afutwe.Hayo yaliba...
kitaifa
Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi alipokuwa anazungumzia ripoti ya utafiti wa watalii walioingia nchini mwaka 2014.Alisema utafiti huo ulifanywa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS...
uchumi
MKUU wa wilaya ya Arusha, Fabian Daqaro (pichani) amewakaribisha wawekezaji katika sekta ya burudani ili kuvutia watalii na kusaidia viwanda vya ndani vinavyozalisha vinywaji vikali na vilaini kuimarisha masoko yao ya ndani.Rai hiyo ameitoa jijini Arusha wakati alipozindua Klabu Mpya yenye hadhi ya kimataifa ya Cocori...
michezo
KINARA wa mabao Ligi Kuu Bara, Salim Aiyee wa Mwadui hajajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars chini ya kocha Emmanuel Amunike, suala ambalo amekiri limezidi kumuongezea hasira na changamoto ya kufanya vizuri zaidi ili wakati mwingine ajumuishwe katika kikosi hicho.Aiyee, ambaye ana mabao 15 dhidi ya ...
michezo
BEKI ya Taifa Stars, Erasto Nyoni amesema kwa sasa anaendelea vizuri, hivyo kama kocha Emmanuel Amunike atampanga mechi dhidi ya Kenya, Alhamisi, atacheza bila shida yoyote.Nyoni yupo mjini hapa na Taifa Stars inayoshiriki michuano ya Afcon na juzi alishindwa kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Senegal kutokana na kusumb...
michezo
Maalim alisema hayo katika kikao cha pamoja kilichowakutanisha watendaji wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko pamoja na ZSTC Ikulu mjini hapa.Alisema wakulima kwa sasa hawana sababu ya kuuza karafuu zao kupitia njia ya magendo ambayo ni ya kubahatisha zaidi kama mtu atakamatwa na karafuu hizo.“Nawapongeza sana wak...
uchumi
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Gaston Kikuwi alisema jana kuwa viwango vilivyowekwa na Serikali kwa sasa, siyo rafiki kwa wafanya biashara wadogo, kwani ni vikubwa mno.Alisema wafanyabiashara wameonesha katika utafiti waliofanya, kumudu viwango visivyozidi Sh 20,000 kwa mijini na Sh 10,000 vijijini.Alitaka viwango hivyo ...
uchumi
Washindi hao, walikabidhiwa pikipiki zao jana katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya ofisi za Vodacom zilizoko Mlimani City, Dar es Salaam.Nyangige aliyekuwa kivutio katika makabidhiano ya zawadi hizo, akizungumza jana alisema; “Mimi ni dada wa kazi za ndani sasa nitaendelea kufanya kazi zangu na kumtafuta kijana am...
uchumi
WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema kukamilika kwa Mradi wa Ukarabati Mnara wa Kuongozea Ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Pemba, kutaongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za kuongozea ndege na usalama wa sekta.Mradi huo umegharimu Sh.milioni 3.1 zilizotolewa na serikali kupitia Mamlaka ya Usalama wa Anga Tanzan...
kitaifa
SERIKALI hupoteza Sh bilioni 31.8 kila mwaka kutokana na uvuvi haramu katika bwawa la Nyumba ya Mungu, linalozungukwa na Halmashauri za Simanjiro mkoa wa Manyara, Moshi na Mwanga mkoani Kilimanjaro.Bwawa hilo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 140 lina uwezo wa kuzalisha tani 5,173 za samaki kwa mwaka zenye thamani ya ...
kitaifa
MAWAZIRI sita wametoa maazimio tisa, yanayolenga kuuokoa Mkoa wa Kigoma dhidi ya uharibifu wa mazingira, ambao tayari athari zake zimeanza kuonekana na kusababisha madhara.Wamesema operesheni hiyo itachukua miezi sita kuanzia sasa, ambayo wanaofanya shughuli za kibinadamu kwenye hifadhi, wanapaswa kuondoka kwa hiari k...
kitaifa
['Inter Milan imefungua mazungumzo na Manchester United kuhusu kiungo wa Chile Alexis Sanchez, mwenye umri wa miaka 30, na wanataka kukamilisha mkataba wa mkopo katika siku tatu zijazo. (Mirror)', 'Barcelona imewasilisha ombi jipya kwa mshambuliaji wa kiungo cha mbele wa Paris St-Germain na wa timu ya taifa ya Braz...
michezo
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imefanikisha kutopeleka mgonjwa wa moyo kwenda nje ya nchi kwa matibabu kwa mwaka huu.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa taasisi hiyo, Dk Peter Kisenge alisema hayo ni mafanikio makubwa kwa taasisi hiyo kwani imesai...
kitaifa
Rais John Magufuli ameingilia kati suala la rangi ya njano kwenye bendera na matumizi ya wimbo wa Taifa, mambo ambayo yamekuwa gumzo mitandaoni kwa siku za hivi karibuni.Taarifa rasmi kutoka Ikulu leo mchana, Rais Magufuli ameeleza kuwa amefuta mara moja maelekezo ya barua iliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Te...
kitaifa
["Chelsea itazishinda Manchester United na Liverpool katika kinyang'anyiro cha usajili wa winga wa England Jadon Sancho, 19, kwa sababu wako tayari kufikia dau la £120m iliyotolewa na Borussia Dortmund. (Sun on Sunday)", 'Mikel Arteta amekubali kuwa kocha mkuu wa Arsenal baada ya kukosa kupata hakikisho kutoka kwa Man...
michezo
WATOTO mapacha wa Elmenesia na Anisia Benatus, wanaendelea vema na tayari wametengenezewa miguu ya bandia. Pacha hao wapo kwenye matibabu nchini Israel, baada ya kutenganishwa, na kila mmoja amebaki na mguu mmoja.Hatua hiyo imewafanya madaktari wa Hospitali ya Riyadhi (pichani) ambao waliwatenganisha, kuwatengenezea m...
kitaifa
Mgahawa huo ulizinduliwa juzi na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dora Msechu.Balozi Msechu alimpongeza Issa Kapande na Nimco Kapande kwa kufanikisha kuwapo kwa mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika katika nchi za Ulaya.Aidha, alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa ku...
uchumi
BARAZA la Uuguzi na Ukunga Tanzania limemsimamisha Martin Chama kutoa huduma za uuguzi na ukunga kwa muda wa mwaka mmoja kwa tuhuma za kufi ka kazini akiwa amelewa na kutaka kuhatarisha usalama wa wagonjwa na ndugu zao kwa kushindwa kutoa huduma kwa umakini na weledi.Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa ...
kitaifa
TAASISI ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) imesema lengo la kuanzishwa kwake mwaka 1981 limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.Mtendaji Mkuu wa Tasuba, Dk Herbert Makoye amesema jana Jijini Dar es Salaam kuwa TaSUBa tangu ianzishwe imepata mafanikio mengi ikiwemo kutoa wataalamu mbalimbali.Alisema hayo katika mahojiano n...
michezo
TANZANIA inahitaji taasisi za moyo kama ya Jakaya Kikwete (JKCI) 10 hivi, ili kukabiliana na tatizo la moyo nchini. Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa JKCI, Naiz Majani alisema hayo jana alipokua akitambulisha mashindano ya marathoni yatakayofanyika kesho katika fukwe za Coco jijini Dar es Salaam.“Tanzan...
kitaifa
Salum aliyasema hayo jana jijini hapa wakati akizungumza kwenye mkutano Taasisi ya Kodi Barani Afrika (ATI) ulioshirikisha wadau wa kodi kutoka nchi 19 barani Afrika pamoja na wawekezaji kutoka nchi za nje wanaokutana kwa siku tatu kwa ajili ya kujadili masuala ya ukusanyaji wa kodi na kuongeza mapato.Alisema Tanzania...
uchumi
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa kushirikiana na serikali inaendelea kujadiliana na wawekezaji wa bandari mpya ya Mbegani- Bagamoyo ili kuangalia namna bora zaidi ya kuinufaisha serikali kimapato.Ujenzi wa bandari hiyo utakapokamilika itaongeza uwezo wa kuhudumia shehena ziingiazo nchini na ziendazo...
uchumi
RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kuufanya Mwaka Mpya wa 2019 kuwa mwaka wa kazi kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali kama vile kilimo, biashara, uvuvi na nyinginezo ili kujiletea maendeleo.Alitoa mwito huo kwenye mkesha wa Kitaifa wa kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2019 uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ila...
kitaifa
VIONGOZI wa kitaifa wametakiwa kufanya kazi kwa pamoja na kuvumiliana kwani huo ndio msingi wa kufikia maendeleo ya kweli. Wito huo ulitolewa jana na Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Central Tanganyika (Dodoma), Dk Dickson Chilongani, katika mahubiri ya Krismasi yaliyofanyika kanisa kuu la Roho Mtakatifu.Ask...
kitaifa
KOCHA wa Singida United, Ramadhan Swanzurimo amesema wamejipanga kimbinu kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya bingwa mtetezi Simba unaotarajiwa kuchezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.Singida wametangaza kutumia uwanja huo kwa michezo miwili ya ligi hiyo dhidi ya Simba na JKT ...
michezo
JAMII imetahadharishwa dhidi ya watu wanaotumia eneo la imani, kwa ajili ya kujinufaisha. Pia, wale wanaojitoa kiimani, wametakiwa kutambua hawafanyi hivyo kwa manufaa binafsi.Hayo yamesemwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza. Alisema hayo ...
kitaifa
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amefunguka kuwa tayari amepata dawa ya kumaliza tatizo la safu ya ulinzi kuruhusu kufungwa mabao kabla ya mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo keshokutwa.Katika mchezo uliopita wa Ngao ya Jamii uliozikutanisha Simba na Azam FC ambao ulimalizika kwa w...
michezo
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Simba leo wanatarajiwa kuwakaribisha Stand United katika mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa taifa, Dar es Salaam.Wachezaji wa Simba wanatarajiwa kuonyesha morali ya hali ya juu kutokana na kupatikana kwa mwekezaji wake Mohamed Dewji ‘Mo’ baada ya kutekwa kwa wiki moj...
michezo
NEEMA sasa imeifikia Halmashauri ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe baada ya mgodi wa makaa ya mawe wa Kabulo uliopo wilayani hapa kuanza kufanya kazi.Kampuni ya CMG Limited ndiyo iliyoingia mkataba wa miezi sita wa kuchimba makaa ya mawe kwenye mgodi huo wa wazi ulio chini ya Shirika la Taifa la Madini (Stamico).Waziri...
uchumi
['Mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 24, hatotia saini kandarasi ya £450,000 kwa wiki hadi pale atakapothibitisha kuwa mkufunzi Pep Guardiola atasalia katika klabu hiyo kwa kipindi cha muda mrefu. (Sun on Sunday)', 'Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anaamini hatowasajili wach...
michezo
JENGO la tatu la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) limekabidhiwa rasmi kwa serikali tayari kwa matumizi baada ya ujenzi wake kukamilika.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Julius Ndyamukama amesema jana mkandarasi alikabidhi kwa Wakala wa Barabara (Tanroads) na kisha...
uchumi
Mkopo huo unalenga kuwezesha waendesha bodaboda wa Dar es Salaam kukua, kuinuka kimtaji na kumiliki bodaboda zao kwa kuwa wengi si za kwao bali wameajiriwa.Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa alisema hayo baada ya kutiliana saini ya makubaliano ya kudhamini NSSF kutoa mikopo kwa Dabosa itoe mikopo kwa wanachama wake....
uchumi
['Manchester United inaweza kushawishika kujaribu kumrejesha tena mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic katika Old Trafford.', ' Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 38- -mchezaji wa kimataifa wa Sweden atakuwa huru kutokana na kwamba mkataba wake na klabu ya ligi ya MLS - LA Galaxy unakaribia kumalizika. ', '(TuttoMercato...
michezo
Kamishna Mkuu wa TRA nchini, Charles Kichere amesema katika taarifa yake kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara atakayebainika kusafirisha bidhaa kwa magendo na kukwepa kodi nchini.Amewataka wafanyabiashara hao kuacha mara moja vitendo hivyo vinginevyo mali zao zote zitakazokamatwa na chombo...
uchumi
MASHINDANO ya Vyama vya Michezo kwa Shule za Msingi na sekondari kwa nchi za Afrika Mashariki (Feasssa) yanaanza leo jijini hapa huku wenyeji Tanzania wakiahidi makubwa.Timu za Tanzania kutoka maeneo mbalimbali tayari zimewasili jijini hapa na kuweka kambi katika shule ya Trust St. Patrick kwa ajili ya kushiriki miche...
michezo
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo ameitaka ofisi ya takwimu kukokotoa vizuri pato la mkoa kupitia viwanda ili mchango wake uonekane na kuutoa mkoa huo kwenye nafasi tatu za mwisho kitaifa.Aliyasema hayo mjini Kibaha wakati wa kikao cha ushauri cha mkoa RCC na kusema kuwa ofisi hiyo inapaswa kufanya tathmini kwani...
uchumi
NAIBU Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini kuwa wazalendo na waaminifu kwa nchi kwa kulipa kodi stahiki zinazotokana na biashara ya madini wanayoifanya.Biteko alisema hayo juzi mjini hapa wakati akifungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika eneo la Katente. Alisema anashangazwa kuona mc...
kitaifa
Ngoma aliwaweka roho juu, mashabiki na wanachama wa Yanga kufuatia habari kuwa, angesaini juzi kuichezea Simba kiasi cha Yanga kudaiwa ‘kumteka’ uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) aliporejea kutoka kwao.Habari zilizopatikana jana kutoka kwa Kaimu Msemaji wa Yanga, Anderson Chicharito zilisema Ngoma ...
michezo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalumu ya SMZ, Haji Omar Kheir alisema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi kwa tiketi ya CUF, Saleh Nassor Juma aliyetaka kujua lini Serikali itajenga soko la kisasa ili kuepuka wafanyabiashara wa mnada wa samaki kufanya shughuli zao katika ma...
uchumi
MFUMUKO wa bei nchini umeongezeka kwa pointi moja kutoka 3.0 Februari hadi 3.1 Machi, mwaka huu.Akizungumza na vyombo vya habari, jijini hapa, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraimu Kwesigabo alisema mfumko wa bei umeongezeka kidogo.Amesema kuongezeka kwa mfumuko w...
uchumi
['Bruno Fernandes, 25, ameambia Sporting Lisbon anataka kujiunga na Man United na mazungumzo zaidi yamepangwa wiki hii baada ya kugonga mwamba kuhusu thamani ya mchezaji huyo wa Portugal. (Sky Sports)', 'Beki wa Paris St-Germain na Ufaransa Layvin Kurzawa, 27, atajiunga na Arsenal kwa uhamisho wa bila malipo wakati kan...
michezo
KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba ana ushawishi unaowaweka watu pamoja klabuni hapo, kwa mujibu wa mchezaji mwenzake Juan Mata.Kumekuwa na tetesi kuhusu Pogba kutaka kuondoka Old Trafford baada ya kusema anatafuta fursa mpya Juni, huku wakala wake akisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anataka kuondoka.M...
michezo
['Kundi la vijana wa Mexico linafufua mchezo wa jadi wa mpira uliowahi kuchezwa na jamii za Aztecs, Maya and Incas.', "Mchezo wa 'Ulama' ulichezwa huko Mesoamerica zaidi ya karne tano zilizopita kabla ya watawala wa Uhispani kuwasili katika eneo hilo mnamo 1519.", 'Wachezaji wanaovaa mikanda maalum na vitambara vy kuj...
michezo
VINARA wa Ligi Kuu Bara, Yanga jana waliingia kwa shangwe mjini hapa baada ya kupata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki na wanachama wake.Mashabiki hao waliipokea timu hiyo mpakani mwa Kilimanjaro na Arusha kwa maandamano ya magari na waenda kwa miguu ambapo walizunguka karibu jiji zima la Arusha na viunga vyake.Ya...
michezo
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeeleza kuongezeka kwa joto juu ya wastani kufi kia nyuzi joto 34 na litadumu mpaka Januari mwakani kutokana na kuwapo kwa jua la utosi na mvua hafi fu za vuli.Imeeleza kuwa wastani wa joto Novemba na Desemba ni nyuzi joto 31.5 kwa mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Ung...
kitaifa
WINGA nyota wa timu ya Bandari na timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Abdallah Hassan amethibitisha kufuatwa na vigogo vya soka vya Tanzania, Simba na Yanga vikitaka kumsajili.Hata hivyo, Hassan hajasema kama yuko tayari kwenda kucheza soka katika timu ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Alisema ni jambo la kawaida kwa ...
michezo
ALIYEKUWA Meneja wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) tawi la Mkwepu, Dar es Salaam Priscus Shirima (37), amefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka ya matatu, ikiwemo utakatishaji fedha Sh milioni 120.Shirima alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mfaw...
kitaifa
Kocha wa timu hiyo Jurgen Klopp amesema kuwa amefurahishwa sana na matokeo hayo, kwani yanazidi kuiweka Liverpool katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo.Washambuliaji wao, Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane wote walizifumania nyavu katika kipindi cha pili katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja ...
michezo
TANZANIA imeendelea kuwa juu katika sekta ya utalii Afrika Mashariki (EAC) kwa kuingiza kipato kikubwa, baada ya kuingiza dola za Marekani bilioni 2.4 mwaka jana.Mapato hayo ya Tanzania ni mbele ya Kenya, iliyoingiza dola za Marekani bilioni 1.55, sawa na takribani shilingi za Kenya bilioni 157.Aidha, watalii walioing...
uchumi
KESHO Jumamosi wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, Simba itakuwa uwanjani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR C) kuvaana na wenyeji wao AS Vita Club.Mchezo huo wa Kundi D ni wapili kwa kila timu baada ya michezo ya awali, ambapo Simba walipata ushindi wa mabao 3-0 mbele ya JS...
kitaifa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa mwito kwa Watanzania kumuenzi Askofu mstaafu, Gabriel Mmole (80) wa Jimbo Katoliki Mtwara kwa wema, upole na utumishi mwema wakati wote wa maisha yake.Alitoa mwito huo jana wakati wa maziko ya Askofu huyo yaliyofanyika ndani ya Kanisa la Watakatifu Wote la mjini Mtwara na kuhudhuriw...
kitaifa
TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), inawashikilia watu watatu akiwamo Diwani wa Kata ya Ukonga wilayani Ilala Mkoa wa Dar es Salaam, Jumaa Mwipopo na Ofi sa Mtendaji wa kata hiyo, Rozalia Silumbe kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Sh 400,000 kwa mwananchi aliyetuhumiwa kufanya uharibifu wa mazingira.Aidha, i...
kitaifa
MAOFISA wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamefanikiwa kumkamata muagizaji wa jumla wa nguo za ndani za mitumba zilizopigwa marufuku kutumika nchini kwa mujibu wa Sheria ya Viwango namba 2 ya mwaka 2009. Kukamatwa kwake ni mafanikio makubwa kwa maofisa wa TBS kwani kupitia msako huo, wengi waliokamatwa ni wachuuzi ...
kitaifa
WAFANYAKAZI wa serikali watalazimika kuwa na subira mpaka kufi kia ndoto ya misha- hara yao kupanda. Hiyo ni kutokana na serikali kushindwa kuweka katika bajeti yake fedha mahususi kwa ajili ya ongezeko la mishahara.Wabunge walio katika Kamati ya Bajeti waliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kutokana na kushindwa...
kitaifa
WATANZANIA wanaotumia dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARVs) wametakiwa kuendelea kutumia pasipo kuacha ili waweze kuishi maisha yenye afya iliyoimarika.Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Anthony Mavunde ameyasema hayo wakati anafungua kongamano la kitaifa la Ma...
kitaifa
Mwenyekiti wa wa Taasisi ya Dk Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi amezindua Maktaba ya Shule ya Msingi Tandale Magharibi, Dar es Salaam na kutoa wito kwa wanafunzi kuitumia vyema maktaba hiyo kujenga maarifa.Aidha amewataka wanafunzi kuilinda maktaba hiyo kama chanzo cha maarifa na weledi. Maktaba hiyo imewezeshwa na taasi...
kitaifa
WAISLAMU nchini wametakiwa kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwao na Watanzania wote ili kulifi kisha taifa kwenye maendeleo ya kweli. Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Rais John Magufuli kwenye maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata).Rais Magufuli ambaye alikuwa mgeni rasmi...
kitaifa
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Stella Ikupa amesema alichokipenda katika matembezi yake kwenye maonesho ya Utamaduni ya Jamafest ni kuona namna wasanii wenye ulemavu wakionesha ubunifu wao wa kutumia vifuu vya nazi kutengeneza pochi.Ikupa alitembelea maonesho hayo...
michezo
WATENDAJI wazembe na watoro wa kuhudhuria vikao vya kisheria, ambavyo vipo kwenye ratiba ya mwaka mzima katika ngazi ya mkoa na wilaya, wameonywa kuacha tabia hiyo.Onyo hilo limetolewa jana jijini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) na kusisitiza kuwa...
kitaifa
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema kuwepo kwa mabaraza ya biashara lengo lake kubwa ni kukuza uchumi na kuibua changamoto zinazokwamisha maendeleo ya sekta hiyo.Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Hassan Khamis Hafidh wakati akizindua Baraza la Biashara la Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja...
uchumi
TIMU ya Taifa ya soka ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, ‘Tanzanite’ leo inashuka kwenye Uwanja wa Taifa kusaka ushindi katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Uganda.Mchezo huo wa kwanza Tanzanite inahitaji matokeo mazuri kuhakikisha inajiweka pazuri kabla ya kwenda kurudiana nao ugenini baadae nchini Uga...
michezo
Imeelezwa kuwa madini hayo hupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), hivyo hukaguliwa na kusimamiwa ipasavyo.Hayo yalibainishwa mjini hapa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliakim Maswi alipotembelea na kukagua maendeleo ya mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka unaoendeshwa kwa ubia kati ya Kampuni ya Australi...
uchumi
NAIBU Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa ameliambia Bunge kuwa ndani ya miezi sita ijayo Wizara ya Kilimo itakamilisha utaratibu wa usajili wa wakulima wa mazao mbalimbali nchini.Pia amekiri kuwa viungo vya chakula (spices) ni muhimu katika afya hususani kwa wanaume na kusisitiza kuwa watatumia faida hizo kuimarisha...
kitaifa
IKOSI cha Simba kimeingia kambini jana tayari kujifua na mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya UD Songo inayotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumapili ya wiki hii.Katika mechi hiyo ya raundi ya awali, Simba inahitaji ushindi kusonga mbele baada ya kutoka suluhu ugenini Beira, Msumbiji w...
michezo
WABUNGE wamesisitiza haja ya serikali kuboresha huduma za matibabu katika hospitali, vituo vya afya na zahanati ili kulinda maisha ya Watanzania hususani wa vijijini na wasio na uwezo.Kwa nyakati tofauti, wakichangia bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na kupongeza juhudi za s...
kitaifa