input stringlengths 5 25.1k ⌀ | label stringclasses 6
values |
|---|---|
TANZANIA imefanya maboresho makubwa na kutengeneza mazingira rahisi ya uwekezaji kwa ajili ya mtu yeyote kuwekeza nchini bila usumbufu. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameliambia Bunge jana kwamba miongoni mwa mazingira hayo ni pamoja kuweka mfumo wa kielektroniki, unaowezesha wawekezaji kuomba leseni, ardhi na ithibati ... | KITAIFA |
NA AMON MTEGA-SONGEA JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Patrick Malindisa (29) mkazi wa Mtaa wa Namanyigu Manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Athanasi Malindisa (70) kwa kumpiga na kitu chenye ncha kali kichwani na kidevuni na kisha kutaka kuufukia kwenye shimo alilochimba ndani ya nyumba y... | KITAIFA |
JANETH MUSHI-ARUSHA KIGOGO anayefanya kazi katika Taasisi ya kusimamia na
kudhibiti Viuatilifu Tanzania(TPRI),Aristerico Silayo, anayedaiwa kumbaka mtoto
wake amekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa baada ya Mahakama ya Hakimu
Mkazi Arusha kuamuru shauri lililokuwa likimkabili lianze upya. Mahakama hiyo jana ilipanga... | KITAIFA |
DORTMUND, UJERUMANI SHABIKI wa klabu ya Borussia Dortmund, amefariki dunia juzi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mainz 05, kwenye Uwanja wa Signal Park. Katika mchezo huo, Dortmund ilifanikiwa kushinda mabao 2-0 ambayo yalifungwa na Marco Reus pamoja na mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United, Shinji ... | MICHEZO |
LONDON, ENGLAND NYOTA wa zamani ambaye aliwika katika klabu ya Liverpool na Tottenham, Jamie Redknapp, amedai bao la mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud, bado halijafikia kuingia katika mabao 20 bora yaliyowahi kufungwa kwenye soka. Giroud amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii wiki hii baada ya kufunga bao mwi... | MICHEZO |
NA JESSCA NANGAWE WAKATI kipa wa Simba, Said Mohammed Nduda akitarajiwa kuondoka wiki ijayo kuelekea India kwa matibabu, beki wa timu hiyo, Shomary Kapombe, atarejea uwanjani kuanza mazoezi mepesi. Kapombe na Nduda ameendelea kukosa mechi za awali za Ligi Luu kutokana na kuwa majeruhi tangu kuanza kwa msimu mpya wa Li... | MICHEZO |
Na IBRAHIM YASSIN-NKASI
MATUMAINI ya kupata mavuno mengi ya mahindi katika Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa, yameanza kupotea baada ya wadudu waharibifu wa mazao aina ya viwavi jeshi kuvamia mashamba ya wakulima na kuyaharibu vibaya.
Wadudu hao wamekuwa wakiharibu zaidi mazao ya mahindi kwa kula majani, kitoto ... | KITAIFA |
Timu ya JKT Tanzania imefanikiwa kuwazuia Mabingwa watetezi wa Simba kuendelea kutamba baada ya kuipachika goli moja kwa bila. Dakika ya 27 ya Mchezo huo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara JKT walifanikiwa kupata goli baada ya Adam Adam kufunga goli la Kichwa. Bao la Adam Adam akiifungua milango ya Simba dakika ya... | MICHEZO |
KATIBU Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mngereza ame- sema Tamasha la Utama- duni la Afrika Mashariki (JAMEFEST) limetoa elimu na kuwanufaisha watu wengi kiuchumi na kisiasa. Akizungumza na gazeti hili Mngereza alisema mbali na wajasiriamali waliotumia fursa kuuza bidhaa zao pia, kuna hoteli na watu w... | MICHEZO |
Mkali huyo aliyetua JKT Ruvu msimu huu akitokea Azam FC, alisema ana imani kubwa na kocha mpya Abdalaah Kibadeni kutokana na uwezo wa ufundishaji aliokuwa nao, hivyo kutua kwake kutabadili mwenendo wao mbovu walioanza nao msimu huu.“Namfahamu Kibadeni ni kocha mwenye uwezo mkubwa wa kufundisha, naamini anaweza kutusai... | MICHEZO |
Promosheni hiyo itakayojulikana kama ‘Pata Patia na NMB’ itadumu kwa miezi sita, ina lengo la kuhamasisha wateja kujiwekea akiba katika akaunti zao na kuweza kujishindia fedha.Kaimu Mkuu Kitengo cha wateja binafsi, Boma Raballa alisema “NMB imeanzisha promosheni hii kwa lengo maalumu la kuhamasisha wateja wake kujiwek... | UCHUMI |
WATENDAJI wa mifuko ya hifadhi ya jamii wametakiwa kuhakikisha wanatii na kutekeleza kwa ufanisi maagizo ya Rais John Magufuli aliyotoa kuhusu wastaafu.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ametoa agizo hilo wakati alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pe... | KITAIFA |
NA KULWA MZEE
-DAR ES SALAAM MFANYABIASHARA Yusufali Manji (41), anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, amekataa mbele ya mahakama kutetewa na Wakili Peter Kibatala, kutokana na kile alichosema ni sababu za kisiasa. Manji alitoa kauli hiyo jana mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Isaya Arufani, kabla hajatoa uamuzi ... | KITAIFA |
Simba na Yanga zinatarajiwa kumenyana Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara.Ninja, ambaye katika mechi za hivi karibuni amekuwa akicheza kwa kiwango kikubwa, aliliambia gazeti hili jana kuwa kukutana na Simba kwake si mara ya kwanza hivyo anaifahamu presha ya... | MICHEZO |
BUNGE limepitisha azimio la kumfungia Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge baada ya kukutwa na kosa la kutoa kauli aliyoithibitisha kuwa Bunge ni dhaifu.Kutokana na uamuzi huo, Lema hatashiriki Mkutano wa 15 ambao ni Mkutano wa Bajeti unaoendelea sasa, Mkutano wa 16 utaka... | KITAIFA |
RAIS John Magufuli amesema serikali itaendelea kumuenzi mgunduzi wa madini ya tanzanite, Jumanne Ngoma pamoja na kazi zake nzuri na amesisitiza kuwa Mzee Ngoma ni shujaa wa taifa.Ahadi hiyo ilitolewa wakati wa maziko ya mzee huyo, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki, nyumbani kwake katika kijiji cha Makanya wilaya ya Same... | KITAIFA |
RABAT, MOROCCO UFALME wa Morocco umelaani vikali vitendo vya Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma, unayeamini anahujumu maombi ya taifa hilo kurejea katika umoja huo. Mfalme Mohammed VI alitangaza rasmi nia ya Morocco kujiunga tena Umoja wa Afrika (AU) wakati akitoa hotuba nchini Rwanda Julai 17... | KIMATAIFA |
Mbunge wa Kahama Mjini (CCM) Jumanne Kishimba ameiomba Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itoe msamaha kwa watu wenye bangi waisalimishe Polisi iuzwe huko Serikali ipate mapato.Amesema Wizara hiyo inaweza kutoa msamaha kwa miezi sita kwa bangi iliyopo kama inavyofanywa kwenye silaha ili bangi hiyo iuzwe kwa usimamizi wa... | KITAIFA |
MWANAMITINDO mwenye jina kubwa nchini Kenya, Annabel Onyango na meneja wa kundi la muziki la Sauti Sol, Marek Fuchs, wanataraji kufunga ndoa ya kihistoria nchini hapo. Kwa mujibu wa mtandao wa Kenyamoja, wachumba hao wa muda mrefu watafunga ndoa hiyo Septemba 19 na sherehe itafanyika katika hoteli ya Great Rift Valley ... | BURUDANI |
Msanii wa Bongofleva hapa nchini, Gigy Money, ametoa dongo kwa baadhi ya watu ambao walikuwa wanamdharau na kumchukulia poa wakati anaanza kazi ya muziki. Gigy Money ameieleza EATV na EA Radio Digital, kuwa ilifika hatua watu wanamsema na kumshambulia mitandaoni pia walijaribu kumchonganisha na Serikali ili mradi wamsh... | BURUDANI |
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Khamis Ali Mzee katika hafla ya ufunguzi wa makocha wa leseni C ya wiki mbili inayofanyika kwenye Uwanja wa Amaan mjini Unguja.Mzee alisema kukamilika kwa mfumo huo kutapelekea kuonesha hali ya michezo yote ya Zanzibar inavyoendelea.Alisema suala la kuandaa mfumo... | MICHEZO |
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Soka Tanzania bara Simba wameendelea kutembeza kichapo kwa kile anayekatiza mbele yao na kuzidi kujihakikishia nafasi ya kutwaa tena ubingwa. Katika uwanja wa Taifa leo ulipigwa mchezo kati ya mabingwa hao na anayewafuata katika msimano mwaka huu Azam Fc. A post shared by Azam Sports (... | MICHEZO |
Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru mke wa bilionea Msuya, Miriam Msuya na mwenzake, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kugoma kuifanyia mabadiliko hati ya mashtaka ingawa alipewa siku tatu kufanya hivyo.
Uamuzi huo ulitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey... | KITAIFA |
MOSCOW, URUSI MAANDALIZI yameanza kwa mkutano utakaowakutanisha wawakilishi kutoka Urusi na Mshauri Mkuu wa Masuala ya Usalama wa Marekani, John Bolton, ambao unatarajiwa kufanyika wiki ijayo mjini Geneva nchini Uswisi. Taarifa hiyo imetolewa jana mjini hapa na msemaji wa Ikulu, Dmitry Peskov. Alisema kila kitu kina... | KIMATAIFA |
JOTO la wabunge wa upinzani kuvihama vyama vyao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), linazidi kuongezeka baada ya Mbunge wa Jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA,) Marwa Chacha kutangaza kukihama chake na kujiunga na chama tawala.Hatua ya Chacha inafikisha idadi ya watano wakiwemo ... | KITAIFA |
“HUDUMA tunazotoa ni nzuri na zina hadhi ya kimataifa. Abiria hachukui zaidi ya dakika saba kukaguliwa na abiria anayewasili anachukua dakika tatu kupata huduma za uhamiaji hadi anatoka nje ya jengo.”“Kwa Watanzania wenye pasipoti za kielektroniki, wanatumia sio zaidi ya sekunde 15 kwa sababu wanajihudumia wenyewe kup... | KITAIFA |
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema haijakatazwa mtu kumiliki zaidi ya kadi moja za simu ilimradi ziwe za mitandao tofauti.“Tunatamani kila Mtanzania awe na ‘line’ moja ya simu kwa mtandao mmoja, akitaka nyingine atoe taarifa,” amesema.Nditiye ameyasema hayo bungeni wakati wa kip... | KITAIFA |
Na JENNIFER ULLEMBO RIADHA ni moja ya michezo inayopendwa duniani kwa asilimia kubwa, kwani mbali na kuwapa watu fedha kwa kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali, pia umekuwa ukisaidia kuimarisha na kutunza afya. Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) lilianzisha mpango wa kuandaa mashindano katika baadhi ya mikoa kw... | AFYA |
Na ANDREW MSECHU -DAR ES SALAAM IKIWA imebaki miezi michache kuelekea Uchaguzi Mkuu, Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk
Ali Mohamed Shein, ametoa onyo kwa watu wanaotaka kuvuruga amani na katu
serikali hatomvulia mtu yeyote kwa kisingizio cha kudai haki. Kutokana na hali hiyo amesema kwa sasa ... | KITAIFA |
WAKUU wa Mikoa ya Tabora na Geita, wamesema Jukwaa la Fursa za Biashara lililofanywa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) katika mikoa yao, limesaidia kuwajengea wananchi na wawekezaji uelewa kuhusu fursa za biashara na uwekezaji katika mikoa hiyo.Katika Mkoa wa Geita, jukwaa hilo la fursa za biashara na uwekezaji... | UCHUMI |
Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amesema kuanzishwa kwa mradi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kutasaidia kukuza uchumi wa nchi. Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga, amesema mradi huo ambao ulianzishwa na Kampuni ya Raddy Fibre Solution (LTD) unatarajiwa k... | KITAIFA |
Na Esther Mnyika, Dar es Salaam MBUNGE wa Ubungo, Saeed Kubenea (Chadema), amesema chama hicho hakitamvumilia kiongozi yeyote anayetaka kurudisha nyuma harakati za kuleta maendeleo na kuwataka wananchi wa jimbo hilo kutoa taarifa za kiongozi anayekwenda kinyume cha taratibu ili aweze kuchukuliwa hatua. Akizungumza na ... | KITAIFA |
Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema Nape amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo litaanzia Geita Machi 26 na kumalizikia Kahama Machi 28.“Maandalizi kuelekea Tamasha la Pasaka yanaendelea vema na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa wazi... | MICHEZO |
BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) katika kujiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwakani, limewataka Waislamu nchini kama sehemu ya Watanzania, kujitokeza kwa wingi katika hatua zote za mchakato utakapoanza ikiwamo kushiriki kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura, kugombea na kuchagua.Aidha, Ba... | KITAIFA |
Hatua hiyo ya kutenga ekari 160 katika eneo la Jitegemee, upande wa barabara ya Mandela inayolenga kuongeza ufanisi wa bandari hiyo kubwa hapa nchini na kuifanya kuwa shindani.Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe alitangaza hatua hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kuhitimisha ziara ya u... | UCHUMI |
Rais wa Sudan, Omar Al- Bashir anadaiwa kuwa tayari kuandaa mazungumzo ya amani kati ya mahasimu wawili wakuu wa Sudan Kusini, Rais Salva kiir na Riek Machar. Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Sudan ilitangaza kwamba ilitangaza pendekezo la Rais Bashir liliwasilishwa kwa Rais Kiir na ujumbe wa Sudan uliotembelea Juba ... | KIMATAIFA |
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema ukosefu wa uadilifu ni eneo ambalo lilitia doa utendaji wa sekta binafsi hususani pale ambapo ilishirikiana na Serikali.Ameyasema hayo wakati anafungua Mkutano Mkuu wa 18 wa mwaka wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa niaba ya Rais John Magufuli.Katika mkutano huo uliofan... | KITAIFA |
Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) linatekeleza mchakato wa marekebisho ya katiba na limetoa siku 30 kwa wadau na wanatasnia ya filamu nchini kutoa maoni yao kwa rasimu ili kuwa na katiba yenye tija kwa tasnia hiyo. Rasimu ya TAFF iliundwa na kupelekwa kwa wadau na baada ya kikao cha utendaji kazi kati ya Bodi ya Fi... | MICHEZO |
OFISA Usalama wa Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe (44) na mwenzake, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa mashitaka mawili likiwamo la kusafi risha dawa za kulevya aina ya heroin.Mbali na Mwamgabe, mshitakiwa mwingine ni Abdulrahman Msimu (54) ambaye ni dereva na mka... | KITAIFA |
Na John Dande -Dar es Salaam WAKAZI zaidi ya 500,000 wanatarajia kulipwa fidia kupisha mradi wa ujenzi wa Mto Msimbazi ili kuepusha madhara yanayotokea wakati wa mvua. Akizungumza mjini hapa jana wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua madhara yanayotokea kwa wanaoishi pembezoni mwa mto huo pindi mvua zinaponyesha, ... | KITAIFA |
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amewataka viongozi na wawakilishi vya vyama vya siasa, kuhakikisha wanatoa maoni yenye tija ili kutengeneza kanuni zilizo bora, zitakazosimamia uchaguzi wa serikali za mitaa.Aidha, Jafo amesema uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajia ... | KITAIFA |
Na Eliza Hombo, Dodoma
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekuwa ikiwatesa na kuwasumbua wafanyabishara hasa katika miji mikubwa ya Dar es Salaam, Arusha na Mbeya.
Lema alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akiuliza swali la papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Kassim... | KITAIFA |
Lyon ilifungwa mabao 4-0 na Azam FC katika michuano hiyo Jumatatu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.Akizungumza na gazeti hili, Salvatory kiungo wa zamani wa Yanga, alikiri kuzidiwa mbinu na Azam FC na kusema wanajipanga kuhakikisha wanashinda michezo yao iliyobaki ili wapande Ligi Kuu.“Tumeondolewa kwenye Kombe la Shir... | MICHEZO |
Na Upendo Mosha, Moshi
HOSPITALI za mikoa ya Kanda ya Kaskazini, zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu salama kutokana na mwamko mdogo wa wananchi kujitolea kutoa damu ili kusaidia wagonjwa wenye mahitaji.
Hayo yamesemwa na Ofisa mipango wa damu salama Kanda ya Kaskazini, Faisal Abubakari, wakati wa utoaji... | KITAIFA |
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Mwambusi alisema wanahitaji kupandisha kiwango angalau kifike kwenye asilimia 65 ili wawe katika nafasi nzuri zaidi ya ushindi.“Bado sijaridhishwa na kiwango cha wachezaji, wanatakiwa wapandishe kiwango angalau kifike asilimia 65, tunaweza kuwa katika kiwango ambacho kinatakiwa zaidi,”... | MICHEZO |
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) inaweza kukusanya Sh trilioni 1.7 kwa mwezi endapo itaongeza vyanzo vipya vya kodi, itadhibiti wanaoharibu mashine za kielektroniki (EDF) na itaipa kipaumbele sekta binafsi ambayo ni injini ya uchumi wa nchi.Akichangia bajeti ya Fedha na Mpango, Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwij... | KITAIFA |
CARDIF, Wales BONDIA wa uzito wa juu duniani, Anthony Joshua, leo anatarajia kupanda tena ulingoni kuzichapa na Mcameroon, Carlos Takam, kugombea mkanda wa IBF katika ulingo wa Principality uliopo jijini Cardif nchini Wales. Joshua anapewa nafasi kubwa ya kushinda katika pambano hilo lakini atatakiwa kuwa makini n... | MICHEZO |
Na WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM KIWANGO cha juu kinachoonyeshwa na viungo wa Simba, Luis Miquissone, Francis Kahata, Hassan Dilunga na wengineo, kimezua hofu miongoni mwa timu pinzani za Ligi Kuu Tanzania Bara. Kahata, Dilunga, Clatous Chama wamekuwa muhimili wa Simba katika eneo la kiungo, wakiwa chachu ya mabao ya ti... | MICHEZO |
Na AGATHA CHARLES – Dar es Salaam ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amerejea nchini jana akitokea New York nchini Marekani alikokuwa akipatiwa matibabu. Taarifa za kurejea kwa Kardinali Pengo zilitolewa jana na Askofu Msaidizi wa Jimbo la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa ... | KITAIFA |
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Dar as Salaam, Daniel Chongolo amezindua kampeni kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kulipa kodi ya majengo na kodi ya mabango.Chongolo amesema kampeni hiyo itaenda sambamba na kampeni ya nyumba kwa nyumba ikilenga kuhakikisha wamiliki wote wanalipa kodi kwa wakati kukusanya Sh bilioni sab... | UCHUMI |
Golikipa nambari moja wa klabu ya Mtibwa Sugar Shaban Kado amezitaka mamnlaka za Soka nchini kuangalia uwezekano wa kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye vilabu vya ligi kuu nchini Akizungmza kwenye kipindi ha Sports HQ cha Efm Kado amesema idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni inahatarisha ukuaji wa timu ya taif... | MICHEZO |
Mchezo huo dhidi ya Zambia ni wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa timu za umri huo zitakazofanyika Papua New Guinea mwaka 2016.Akizungumzia mchezo huo jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto alisema wachezaji wote wanaendelea vizuri na wako tayari kwa ajili ya mchezo hu... | MICHEZO |
SERIKALI imeanza kushughulikia mgogoro wa vyama vya ushirika na wawekezaji wa mazao ya kahawa na parachichi wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro na kuahidi mazingira sawa yatakayonufaisha pande zote, ikiwemo ulipaji kodi.Kikao kilichokutanisha pande zote kimefanyika wilayani hapa kuhakikisha vyama vya ushirika, wawekezaji... | KITAIFA |
Na CLARA MATIMO MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea kutenda mema kama walivyotenda wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa kufanya ibada na kuliombea taifa amani. Alitoa wito huo kwa waislamu hivi karibuni katika baraza la Idd EL Fitr kwenye msikiti wa Shia. Alis... | KITAIFA |
MOMBASA, KENYA
SENETA wa Mombasa, Hassan Omar, amemshutumu Rais, Uhuru Kenyatta, kwa kupaisha umaarufu wa Gavana wa kaunti hiyo, Hassan Joho.
Akizungumza na wakazi wa Changamwe kauntini hapa juzi, Omar ambaye anagombea ugavana wa Mombasa alimtaka Rais Uhuru akome kuingilia siasa za Mombasa na kwamba yeye ang... | KIMATAIFA |
Chanzo cha picha, Instagram/Justin Bieber
Mwimbaji Justin Bieber amesema Imani yake kwa Yesu imemsaidia kukabiliana na matatizo ya kimatibabu yaliyomkabili hivi karibuni.
Nyota huyo wa muziki alifichua wikindi iliyopita kwamba anakabiliwa na hali ya kiafya iliyomsababishia kupooza uso wake. Tangazo hilo lilifuatia ku... | AFYA |
JIJI la Dar es Salaam jana lilizizima baada ya kuwasili kwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Dk Reginald Mengi, ambao baada ya kupokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam (JNIA), msafara wake ulipita katika mitaa mbalimbali ya jiji hilo.Dk Mengi alifariki dunia Alhami... | KITAIFA |
Na Ramadhan Hassan, Dodoma Naibu Spika, Dk. Tulia Akson leo amewagomea Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuwasilisha taarifa ya kudumu ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kutokana na kutowasilisha taarifa yao kwa Spika siku moja kabla ya kusomwa bungeni. Kwa mujibu wa waraka wa Spi... | KITAIFA |
NEW YORK, MAREKANI ALIYEKUWA mshindani mkubwa wa mkali wa muziki Afrika Mashariki na Kati, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’, msanii kutoka Uganda, Eddie Kenzo, ndiye aliyeibuka mshindi katika tuzo za Nigeria Entertainment Awards 2015 (NEA) kipengele cha ‘African Artist of The Year’ walichokuwa wakishindania. Mganda huyo ... | BURUDANI |
NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, Hans Van der Pluijm, amesema hafikirii kuwa kupata mabao mengi katika mechi ndiyo kufanya vizuri, yeye anachokiangalia na kukiamini katika kikosi chake ni ubora, hata kama watashinda moja kila mechi. Yanga ilifanikiwa ... | MICHEZO |
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hali ya usalama katika Sikukuu ya Idd Al-Hajj, ilikuwa shwari.Mambosasa amesema kuwa hakukuwa na tukio lolote na kwamba wakazi wa jiji hilo walisherehekea kwa amani na utulivu.Amesema jeshi hilo liliweka ulinzi katika maeneo mbalimbali ili kudh... | KITAIFA |
Na JANETH MUSHI -ARUSHA UAMUZI wa kusikilizwa maombi ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema utajulikana leo mbele ya Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Jaji Sekela Moshi. Jaji Moshi anatarajiwa kutoa uamuzi huo baada ya Mawakili wa Serikali kuweka pingamizi za awali wakipinga ... | KITAIFA |
MANCHESTER, ENGLAND KLABU ya Chelsea inadaiwa ilitoa ofa nono zaidi ya Manchester United ili kumsajili kinda Anthony Martial, taarifa kutoka Ufaransa zimeeleza juzi. Jarida la CanalPlus limesema kuwa straika huyo wa zamani wa Monaco aliipiga chini ofa ya The Blues kwa kuwa alikuwa na ndoto ya kuhamia United, ambayo ili... | MICHEZO |
ALIYEKUWA Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba (pichani) ameingia bungeni kwa mara ya kwanza tangu kuvuliwa wadhifa huo, na kumshukuru Rais John Magufuli kwa kumuamini na kumpa fursa ya kutumikia wananchi.Pia, amemshukuru Spika wa Bunge na Ofisi ya Spika kwa kumpa ushirikiano katika kipindi chote akiwa waziri. Jumamosi... | KITAIFA |
MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imemwita Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dk. Imni Patterson, kujieleza juu ya taarifa wanazozitoa kwenye mitandao yao ya kijamii ikiwamo maambukizi ya corona nchini. Taarifa kwa umma iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushi... | KITAIFA |
Chanzo cha picha, Getty Images
Binadamu wanakabiliwa na vitisho vingi, kuanzia mabadiliko ya hali ya hewa, utapiamlo hadi kupanda kwa gharama ya maisha. Je, maharage yanaweza kuwa jibu la matatizo ya kimataifa?
Jamii hii ya kunde ni sehemu muhimu ya karibu kila utamaduni duniani, na kwa sababu nzuri.
Maharage yakiwa n... | AFYA |
Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM DIRISHA la usajili limefunguliwa rasmi Juni 15 mwaka huu kwa kuziruhusu klabu kusajili, kuuza wachezaji na kuwapeleka kwa mkopo wachezaji ambao wanatakiwa kuongeza uwajibikaji katika timu ili kuakisi ubora unaotakiwa Tangu kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara Mei 20 mwaka huu kumekuwa na ... | MICHEZO |
NEW YORK, MAREKANI MWANAMITINDO maarfu nchini Marekani, Amber Rose, ameonesha jeuri ya fedha kwa kutumia dola 55,000, zaidi ya Sh milioni 121 kumnunulia mpenzi wake saa. Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 33, amethibitisha kuwa kwenye uhusiano na rapa 21 Savage mwenye umri wa miaka 24. Awali rapa huyo alitumia kiasi kam... | BURUDANI |
Na Kulwa Mzee-Dodoma
KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imesema bajeti yao ya mwaka 2017/18 ni ya historia ina kurasa 200 ikiwa na makadirio ya Sh trilioni 29.9.
Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, Halima Mdee, alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mapendekezo ya bajeti ya Serikali mwa... | KITAIFA |
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) pamoja na Chuo Kikuu cha Yale cha Marekani, watatoa tiba ya radiolojia kuanzia Oktoba 22 hadi Novemba 9, mwaka huu.Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ... | KITAIFA |
Suleiman ambaye alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Simba katika miaka ya 1998-2000, ambako alifanya mabadiliko makubwa kiasi cha kupewa jina na aliyekuwa rais wa Urusi, Boris Yeltsin.Wenyeviti wa Simba kwa nyakati tofauti, Ismail Aden Rage na Hassan Dalali walimli... | MICHEZO |
Los Angeles, Marekani MNENGUAJI maarufu nchini Marekani, Black Chyna, jana alionekana jijini Los Angeles, Marekani akitembea kwa kutumia msaada maalumu wa baiskeli ya walemavu. Hata hivyo, haikuwa wazi sababu za mwanadada huyo ambaye alikuwa na uhusiano na Rob Kardashian, kuomba msaada huo ambao hutolewa kwa watu weny... | MICHEZO |
Wakizungumza jana asubuhi walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kutoka katika ziara hiyo ya masomo, viongozi hao walisema mafanikio ya uchumi wa gesi, yatapatikana ikiwa Watanzania watashirikiana na serikali, kuhakikisha wanafikia uchumi wa gesi asilia.Katika kushirikiana huko, vion... | UCHUMI |
Mwandishi wetu, Tanga WAFANYABIASHARA wa Mkoa wa Tanga, wamesema hawaoni shidakulipa kodi baada ya kuona utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleoinayofanywa na Rais Dk. John Magufuli kupitia kodi zao. Hayo yalizungumzwa na wafanyabiashara wakati wa kampeni ya elimukwa mlipakodi inayoendelea mkoani humo ambako maafisa... | UCHUMI |
Kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema itasikilizwa siku tatu mfululizo kuanzia Novemba 27 hadi 29, mwaka huu katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha. Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Devota Msoffe amesema uamuzi huo ni kutokana na kesi hiyo kuwa nje ya wakati. “Tutasikiliza kesi hii s... | KITAIFA |
NA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM TIMU ya Simba imepanga kuwatema nyota wake watatu na kusajili wachezaji wenye uzoefu ili kuimarisha kikosi hicho ambacho kinaundwa na chipukizi wengi. Simba imeanza mikakati ya usajili kwa ajili ya msimu ujao baada ya kumaliza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ikiwa nafasi ya tatu huku ubi... | MICHEZO |
WIZARA, Idara zinazozjitegemea, wakala na taasisi za serikali zote na Serikali za Mitaa zimeagizwa kuhakikisha zinajiunga na mfumo wa Serikali wa Kieletroniki wa Ukusanyaji wa Mapato (GePG) kabla ya Juni 30, mwaka huu.Majaliwa alitoa agizo kwenye hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa 14 wa Bunge la 11 alipokuwa akizung... | KITAIFA |
Kulingana na Shirikisho la Afya ya Akili Dunia (WFMH), asilimia 75 na 95 ya watu wanaokabiliwa na matatizo ya afya ya kiakili katika nchi zenye mapato ya chini na zile za mapato ya wastani hawawezi kupata huduma kabisa.
Hata hivyo asilimia kubwa ya vijana hawana elimu ya kutosha ya afya ya akili, Sasa kijana mmoja ... | AFYA |
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema wachezaji wapya wa timu hiyo, Henrikh Mkhitaryan na Pierre-Emerick Aubameyang, wanahitaji muda kabla ya kuanza kuonesha ubora wao na kuisaidia timu hiyo. Wachezaji hao ambao wamesajiliwa katika dirisha dogo la Januari mwaka huu kutoka Manchester United na Borrusia Dortmund, wali... | MICHEZO |
ALIYEWAHI kuwa msimamizi wa mwonekano wa Diamond Platnumz, ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Q Boy Msafi amesema alilazimika kwenda Afrika Kusini kusomea masuala ya fasheni na muziki kwa kuwa ni vitu vinavyoendana. Akizungumza na Show Biz, Q Boy alisema mwanzoni alikuwa anapenda sana muziki na alifahamu ili kuwa mwa... | BURUDANI |
“NAIPONGEZA timu nzima ya Mkoa wa Arusha iliyobuni mtihani wa pamoja kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa mkoani ambao sasa unasaidia wanafunzi kukuza vipaji vyao na kuwawezesha kuongeza ufaulu zaidi.”Ndivyo anavyosema Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anapozungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango ... | KITAIFA |
NA KULWA MZEE -DAR ES SALAAM MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imekubali kupokea ripoti za mkemia zinazothibitisha kwamba sampuli ya mkojo wa Mlimbwende wa Tanzania 2006, Wema Sepetu, imekutwa na chembechembe za bangi na majani yalibainika kuwa dawa za kulevya aina ya bangi. Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thoma... | BURUDANI |
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Vodacom Tanzania bara wamefanikia kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuwatoa Azamu kwa penati 3 kwa mbili. Katika mechi iliyopigwa usiku wa leo dakika 90 zilimalizika kwa timu zote kutokufungana na baadaye zikaingia hatua ya penati. Kwa matokeo hayo Simba itakutana fainali na M... | MICHEZO |
Na CLARA MATIMO, MWANZA ASKARI mmoja wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, amefariki ghafla akiwa eneo la kazi katika kituo cha Polisi Nyagezi, jijini Mwanza. Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alimtaja askari huyo kuwa ni Koplo Marco Mahona, ambaye alifariki juzi saa saba... | KITAIFA |
WACHEZAJI wa timu ya Tanzania itakayoshiriki Michezo ya 12 ya Afrika itakayofanyika Rabat, Morocco kuanzia Agosti 19 hadi 31 wametakiwa kutokuwa wanyonge kutokana na idadi yao ndogo na badala yake kupambana na kuleta medali.Tanzania katika michezo hiyo inapeleka timu za michezo miwili za riadha yenye wachezaji sita, h... | MICHEZO |
Faraja Masinde, Dar es salaam BARAZA la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO), limemvua nafasi zote za Uongozi aliyekuwa katibu Mkuu wake , Islamil Suleiman. Akizungumza Dar es Salaam leo Januri 25, Mwenyekiti wa NaCoNGO, Nicholaus Zacharia, amesema uamuzi huo ulifikiwa baada ya kikao cha dharura kilichof... | KITAIFA |
Na Mwandishi wetu, Mbeya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara ambao hawajakadiriwa Kodi ya mapato kwa kipindi kinachoishia Marchi 31, mwaka huu kufika katika ofisi za mamlaka hiyo kukadiriwa na kulipa Kodi zao kabla ya Juni 30,2020. Hayo yamezungumzwa leo jijini Mbeya na Kaimu Meneja wa Elimu kwa ... | UCHUMI |
Akitoa maelezo hayo juzi jioni bungeni, mbunge huyo alisema ametumia Kanuni ya 28 (8) ya Kanuni za Bunge za Kudumu.Alisema mashine hizo zimekuwa kero kwa wafanyabiashara na bei ni kubwa, ikilinganishwa na gharama halisi na pia bado matumizi yao hayajaeleweka kwa watumiaji wengi.“Naomba Serikali isitishe uuzaji wa mash... | UCHUMI |
Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM
KATI ya Novemba 25 hadi Desemba mosi, 2017 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), ilifanya upasuaji mkubwa wa moyo wa kihistoria nchini.
Madaktari Bingwa wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Open Heart International kutoka nchini Austraria waliwafanyia upasuaji wagonjwa ... | AFYA |
End of preview. Expand in Data Studio
README.md exists but content is empty.
- Downloads last month
- 3